Saturday, August 8, 2009

YANGA KUUMANA NA MTIBWA SUKARI

Mabingwa wa soka nchini Dar yanga Afrikan wanatarajiwa kuchuana na mtimbwa sukari katika pambano la ngao ya hisani katka mchezo utakaofanyika jumapili wiki ijayo katika uwanja wa uhuru jijini Dar es salaam.

Katibu mkuu wa shirikisho la soka nchini tff Fredrick Lameck Mwakalebela amesema kuwa mchezo huo utakuwa ni sehemu ya maandalizi ya ligi kuu Tanzania bara inayotarajiwa kuanza kutimua vumbi august 23 mwaka huu.

Mwakalebela ameongeza kuwa mchezo wa ngao ya hisani utakuwa unafanyika kila mwaka ikiwa ni sehemu ya kuashiria kufungua kwa msimu wa ligi nchini


TIKETI KUWAONA SIMBA,VILA ZAUZWA
Tiketi kwa ajili ya pambano la simba na spot clab villa ya Uganda zimeanza kuuzwa leo katika vituo mbalimbali vilivyoteuliwa jijini Dar es salaam.

Kiingilio cha juu kabisa katika pambano hilo litakalofanyika kesho katika uwanja wa uhuru kitakuwa shillingi elfu 50 wakatik kile cha chini kitakuwa shilingi elfu 3.

Mwenyekiti wa kamati ya mashindano ya simba Hassan Hassano maarufu kama mpiganaji amevitaja vituo vya kuuzia tiketi kuwa ni katika vituo vya steers, hadees, big bon, millennium tower na maeneo mengine jijini DAR

Hassano ameongeza kuwa maandalizi katika tamasha hilo ambalo lina lengo la kuwatambulisha wachezaji wa simba ikiwa pamoja na kutambulisha jassey watakazotumia katika ligi kuu msimu ujao yamekamilika kwa asilimia kubwa.

Hasano amesema kuwa vifaa kwa ajili ya kupamba tamasha hilo vimewasili kutoka nchini afrika kusini hivyo amewataka mashabiki wa simba kujitokeza kwa wingi kesho uwanjani kushuhudia vitu vilivyoandaliwa na wekundu hao.

Sambamba na hilo clab hiiyo leo imetembelea katika hospitali ya taifa ya muhimbili kwa ajili ya kuwaona wagonjwa katika word ya watoto na wamefanikiwa kutoa zawadi mbalimbali kwa walengwa.


Katibu mkuu wa shirikisho la soka nchini tff Fredrick Mwakalebela amesema kuwa maandalizi kwa ajili ya michezo ya ufukweni inayofadhiliwa na shirikisho la soka ulimwenguni yaani fifa yanaendelea vizuri ikiwa pamoja na wadhamini mbalimbali kuanza kujitokeza

Mwakalebela amesema kuwa kwa sasa wanaandaa viwanja vitakavyotumika kaatika michezo hiyo.

UKATA WA YANGA HATIMAYE WAISHA
Baada ya kilabu ya yanga kuwa katika hali ngumu kiasi cha wapinzani wao kuanza kuwabeza kuwa wamefulia hatimae wachezaji wa wanajangwani hao wamelipwa malimbikizo ya mishahara yao ya miezi miwili.

Mmoja wa wachezaji hao ambae hakutaka jina lake litajwe redioni amesema kuwa kwa sasa karibu wachezaji wote wana ari ya kufanya mazoezi baada ya adui njaa kuanza kuwakimbia.

Ameongeza kuwa amekuwa katika wakati mgumu sana kiuchumi kiasi ambacho hawezi kukielezea na kuongeza kuwa anaushukuru uongozi wao kwa kuweza kulifanyia kazi suaala hilo mapema iwezekanavyo.

Ameongeza kuwa kwa sasa anaamini mazoezi ya wanajangwani hao yataendelea vizuri japo wachezaji sita wa timu hiyo wapo katika kikosi cha taifa stars kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa kirafiki dhidi ya amavubi ya Rwanda utakaofanyika wiki ijayo nchini Rwanda.

Wachezaji hao walikuwa wakidai mishahara yao ya miezi miwili juni na julai hali iliyopelekea kudorola kwa mazoezi hayo na kumfanya kocha mkuu wa timu hiyo Dusan Condic kuwa katika wakati mgumu wa kuendelea na programu yake ya maandalizi ya ligi kuu.

KIFA KUWAPATA KINONDOKE KESHO
Uchaguzi wa chama cha makocha mkoa wa kinondoni kisoka unatarajiwa kufanyika jumapili wiki hii katia ukumbi wa manspaa ya kinondoni huku nafasi ya mweka hazina msaidizi ikiwa wazi kwa kukosa mgombea.

Katibu mkuu wa chama cha soka kinondoni KIFA Frank Mchaki amesema kuwa usaili kwa ajili ya uchaguzi huo umeshafanyika na kupitisha wagombea waliokizi vigezo.

Mchaki amewataja wagombea watakashiriki katika uchaguzi kuwa ni Eliutel Mholela katika nafasi ya mwenyekiti, wakati makamu mwenyekiti ni Cansius Masombora.

Nafasi ya katibu mkuu itagombewa na Mbwana Makata wakati nafasi ya katibu msaidizi yupo Daniel Mashote

Mweka hazina itagombewa na Evarist Katomondo huku nafasi ya mweka hazina msaidizi ikiwa haina mgombea.

Boniface Wambura atagombea nafasi ya mjumbe taifa wakati Hamis Pondamali na Samson Hika wao watagombea nafasi ya mjumbe kamati ya utendaji.

SC VILLA YAWASILI JIJINI LEO

Michezo na burudani 06/08/2009

Timu ya sport klab vila ya Uganda imewasili leo jioni kwa ajili ya mpambano wa kirafiki na timu ya simba utakaofanyika siku ya jumamosi katika tamasha la wekundu hao.

Mweka hazina msaidizi wa simba Chano Almasi amesema kuwa maandalizi kwa ajili ya tamasha hilo yanaendelea vizuri.

AFRICAN LYON KIKICHAPA NA SC VILLA
Baada ya timu ya afrikan lyon kukubali kichapo cha bao 3-0 na timu ya taifa ya vinaja Serengeti boys hapo jana inatarajiwa kuwa na pambano la kupimana nguvu na timu ya sport clab villa ya nchini Uganda.

Akizungumza kwa njia ya simu na kipindi hiki msemaji wa timu ya afrikan lyoni hasan mvula amesema kuwa pambano hilo litafanyika siku ya jumapili wiki hii katika uwanja wa uhuru jijini Dar es salaam.

Mvula ameongeza kuwa kufungwa na timu ya taifa ya vijana hapo jana ni sehemu ya changamoto kwa mwalimu wa timu hiyo kujua wapi anahitaji kufanya marekebisho katika maandalizi ya ligi kuu msimu ujao ambayo inatarajiwa kuanza kutimua vumbi tarehe 23 mwezi huu.

PWANI YAJIPANGA KISOKA
Baada ya timu ya vijana ya mkoa wa pwani kutofanya vizuri katika michuano ya kopa coca cola iliyomalizika hivi karibuni, chama cha soka mkoani humo COREFA kimeandaa mikakati babu kubwa kwa ajili ya kuwaendeleza vijana kwa kuandaa michuano mbalimbali mkoani humo.

Mwenyekiti wa corefa Hassan Hasanoo maarufu kama mpiganaji, amesema kuwa kwa sasa michuano ambayo inaendelea ni ile ya kawambwa cup ambayo inafanyika wilaya ya bagamoyo ikiwa ni sehemu ya kuendeleza soka la vijana mkoa wa pwani.


SIMBA KUWAONA WAGONJWA KESHO
Klab ya simba kesho inatarajiwa kwenda kuwaona wagonjwa katika wodi ya watoto katika hospitali ya mhimbili jijini Dar es salaam.

Mwenyekiti wa kamati ya mashindano ya simba hasani hasanoo amesema wameamua kufanya hivyo kutokana na kuona umuhimu wa wodi ya watoto na changamoto mbalimbali wanazokumbana nazo.

JESHI LA POLISI KUWALINDA CHIWA,MROSO
Jeshi la polis katika kituo cha changombe jijini Dar es salaam, limejipanga vizuri kwa ajili ya kutoa ulinzi katika pambano la ngumi kati ya liston chiwa na Robert Mroso litakalofanyika jumamosi wiki hii katika ukumbi wa luxury pub temeke.

Rais wa organization ya ngumi za kulipwa nchini TPBO Yassin Abdallah amesema kuwa maandalizi kwa ajili ya pambano hilo yanaendelea vizuri ambapo kesho mabondia wote watakaopigana watapima uzito ikiwa ni sehemu ya kukamilisha maandalizi yenyewe.

Stars Kuwafunda Serengeti Boys

Michezo na burudani 04/08/2009

Timu ya taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 wanatarajiwa kuchuana na timu ya taifa ya Tanzania taifa stars ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya michuano ya kombe la vijana la cecafa linalotarajiwa kuanza kutimua vumbi tarehe 18 mwezi huu nchini sudan.

Katibu mkuu wa shirikisho la soka nchini tff Fredrick lameck Mwakalebela amesema kuwa maandalizi kwa ajili ya michuano hiyo yanaendelea vizuri.

TFF YAITUNISHIA MISULI SIMBA
Shirikisho la soka nchini tff limeitunishia misuli timu ya simba kwa kukataa maombi ya wachezzaji wao kujiunga na timu ya taifa baada ya tamasha lao linalotarajiwa kufanyika tarehe 8 mwezi huu katika uwanja wa uhuru jijini dar.

Stars ambayo imeanza mazoezi yake jana bila ya wachezaji 7 wa simba walioitwa kujiunga na timu hiyo kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya wanyarwanda unaotarajiwa kutimua vumbi august 12 mwaka huu nchini Rwanda

Katibu mkuu wa tff Fredrick mwakalebela ameigomea barua yao kwa kuwataka wajiunge na timu hiyo haraka iwezekanavyo kwa kuwa mchezo huo ni kwa maslahi ya watanzania wote na kuwataka waonyesha uzalendo

TAITANIC WAIBUKA KIDEDEA
Timu ya titanic leo imewanyuka home boys kwa jumla ya bao 3-1 katika mashindano yanayoendelea ya kombe la upendo katika mchezo uliofanyika uwanja wa tandika mabatini jijini Dar es salaam.

Taitanic ndio walikuwa wa kwanza kuzifumania nyavu za home boys katika dk 5 tu ya mchezo kupitia kwa Mrisho timam bao lililodumu hadi mapumziko.

kipindi cha pili kilianza kwa timu zote kuonyesha shauku ya kutaka kupata bao na katika 61 maulid kudra aliisawazishia bao timu yake ya home boys hali iliyowapelekea wapinzani wao kuongeza kasi ya mashambulizi kwa lengo la kupata ushindi katika mchezo huo.
Baada ya dk 6 mbele mrisho tamim tena aliipatia timu yake ya titanic bao la pili kabla ya Hebu Gamba kuongeza bao la 3 lililodumu hadi mwisho wa mchezo na kuwafanya home boys waondoke uwanjani kwa kichapo cha bao 3-1.

Kesho ligi hiyo itaendelea tena kwa kuzikutanisha timu ya temeke squad watakaotoana jasho na aman fc katika uwanja huo huo wa tandika mabatini.

Wakati huohuo timu ya sekondari ya magnus inatarajiwa kushuka dimbani kesho kumenyana na timu ya wakuzuka fc katika mchezo wa nusu fainali jez cup katika mchezo utakaofanyika katika uwanja wa majohe

Habari hii ni kwa mujibu wa mweka hazina msaidizi wa chama cha soka la vijana wilaya ya ilala IDYOSA

Kuwaona Villa Elfu Hamsini

Timu ya simba sports club leo imetangaza kiingilio cha kwenye tamasha la timu hiyo itakapopambana na timu ya sport villa ya uganga katika mchezo utakaofanyika jumapili wiki hii katika uwanja wa uhuru jijini Dar es salaam.

Mwenyekiti wa wekundu hao hasan Dalali amesema kuwa kiingilio cha juu kitakuwa shilingi elfu 50 wakatiki kile cha chini kitakuwa shilingi eltu 3

Dalali amesema kuwa siku ya pambano hilo ambalo litakuwa na lengo la kuitambulisha timu ya simba sambamba na kuwatambulisha wachezaji wapya, ambapo mgeni rasimi atakuwa spika wa bungu la jamhuri ya muungano wa Tanzania samwel sitta

Sambamba na hilo club ya simba imelitaka shirikisho la soka nchini tff kuwaruhusu wachezaji waliochaguliwa kucheza timu ya taifa stars kujiunga na timu hiyo augast 9 badala ya siku ya leo kama ilivyokuwa imetangazwa.

Simba waigomea stars
Katibu mkuu wa simba mwina kaduguda amesema kuwa sababu ya kufanya hivyo ni kuwaandaa wachezaji wa klab hiyo katika maaandalizi ya ligi kuu Tanzania bara inayotaarajiwa kuanza kutimua vumbi augast 23 mwaka huu wakiwa chini ya kocha wao.

Wachezaji saba wa timu ya simba walioitwa katika timu ya tafifa ya Tanzania taifa stars ni ally Mustapha, kelvini yondan, david naftari, juma jabu, juma nyoso, musa hasan mgosi na danny mrwanda.


soka
Timu ya davis conner leo imetoa kichapo kwa timu ya mchanagani kwa kuifunga jumla ya boa 2-1 katika mchezo wa ligi ya kombe la upendo uliofanyika katika uwanja wa tandika mabatini jijini Dar es salaam.

Mabao ya davis conner yalifungwa na mashaka mahira katika dk ya 11 na 26 wakati lile la kuondoa aibu la mchangani lilipachikwa wavuni na abuu azizi katika dakika 52.

Ligi hiyo itaendelea tena kesho wakati watani wa jadi wa ligi hiyo wataingia uwanjani kuonyeshana ubabe wa nani mkali kati ya timu ya taitanic sports club na home boys team katika mchezo utakaopigwa pale pale katika uwanja wa tandika mabatini.

Nayo mashindano la kombe la maembe (maembe cup) imeendelea leo hatua ya robo fainali ambapo timu ya ya hali ya hewa imewachapa kitintale bao 1-0 katika mchezo uliofanyika katika uwanja wa shule ya msingi yombo kiwalani.