Saturday, August 8, 2009

SC VILLA YAWASILI JIJINI LEO

Michezo na burudani 06/08/2009

Timu ya sport klab vila ya Uganda imewasili leo jioni kwa ajili ya mpambano wa kirafiki na timu ya simba utakaofanyika siku ya jumamosi katika tamasha la wekundu hao.

Mweka hazina msaidizi wa simba Chano Almasi amesema kuwa maandalizi kwa ajili ya tamasha hilo yanaendelea vizuri.

AFRICAN LYON KIKICHAPA NA SC VILLA
Baada ya timu ya afrikan lyon kukubali kichapo cha bao 3-0 na timu ya taifa ya vinaja Serengeti boys hapo jana inatarajiwa kuwa na pambano la kupimana nguvu na timu ya sport clab villa ya nchini Uganda.

Akizungumza kwa njia ya simu na kipindi hiki msemaji wa timu ya afrikan lyoni hasan mvula amesema kuwa pambano hilo litafanyika siku ya jumapili wiki hii katika uwanja wa uhuru jijini Dar es salaam.

Mvula ameongeza kuwa kufungwa na timu ya taifa ya vijana hapo jana ni sehemu ya changamoto kwa mwalimu wa timu hiyo kujua wapi anahitaji kufanya marekebisho katika maandalizi ya ligi kuu msimu ujao ambayo inatarajiwa kuanza kutimua vumbi tarehe 23 mwezi huu.

PWANI YAJIPANGA KISOKA
Baada ya timu ya vijana ya mkoa wa pwani kutofanya vizuri katika michuano ya kopa coca cola iliyomalizika hivi karibuni, chama cha soka mkoani humo COREFA kimeandaa mikakati babu kubwa kwa ajili ya kuwaendeleza vijana kwa kuandaa michuano mbalimbali mkoani humo.

Mwenyekiti wa corefa Hassan Hasanoo maarufu kama mpiganaji, amesema kuwa kwa sasa michuano ambayo inaendelea ni ile ya kawambwa cup ambayo inafanyika wilaya ya bagamoyo ikiwa ni sehemu ya kuendeleza soka la vijana mkoa wa pwani.


SIMBA KUWAONA WAGONJWA KESHO
Klab ya simba kesho inatarajiwa kwenda kuwaona wagonjwa katika wodi ya watoto katika hospitali ya mhimbili jijini Dar es salaam.

Mwenyekiti wa kamati ya mashindano ya simba hasani hasanoo amesema wameamua kufanya hivyo kutokana na kuona umuhimu wa wodi ya watoto na changamoto mbalimbali wanazokumbana nazo.

JESHI LA POLISI KUWALINDA CHIWA,MROSO
Jeshi la polis katika kituo cha changombe jijini Dar es salaam, limejipanga vizuri kwa ajili ya kutoa ulinzi katika pambano la ngumi kati ya liston chiwa na Robert Mroso litakalofanyika jumamosi wiki hii katika ukumbi wa luxury pub temeke.

Rais wa organization ya ngumi za kulipwa nchini TPBO Yassin Abdallah amesema kuwa maandalizi kwa ajili ya pambano hilo yanaendelea vizuri ambapo kesho mabondia wote watakaopigana watapima uzito ikiwa ni sehemu ya kukamilisha maandalizi yenyewe.

No comments:

Post a Comment