Saturday, August 8, 2009

Stars Kuwafunda Serengeti Boys

Michezo na burudani 04/08/2009

Timu ya taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 wanatarajiwa kuchuana na timu ya taifa ya Tanzania taifa stars ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya michuano ya kombe la vijana la cecafa linalotarajiwa kuanza kutimua vumbi tarehe 18 mwezi huu nchini sudan.

Katibu mkuu wa shirikisho la soka nchini tff Fredrick lameck Mwakalebela amesema kuwa maandalizi kwa ajili ya michuano hiyo yanaendelea vizuri.

TFF YAITUNISHIA MISULI SIMBA
Shirikisho la soka nchini tff limeitunishia misuli timu ya simba kwa kukataa maombi ya wachezzaji wao kujiunga na timu ya taifa baada ya tamasha lao linalotarajiwa kufanyika tarehe 8 mwezi huu katika uwanja wa uhuru jijini dar.

Stars ambayo imeanza mazoezi yake jana bila ya wachezaji 7 wa simba walioitwa kujiunga na timu hiyo kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya wanyarwanda unaotarajiwa kutimua vumbi august 12 mwaka huu nchini Rwanda

Katibu mkuu wa tff Fredrick mwakalebela ameigomea barua yao kwa kuwataka wajiunge na timu hiyo haraka iwezekanavyo kwa kuwa mchezo huo ni kwa maslahi ya watanzania wote na kuwataka waonyesha uzalendo

TAITANIC WAIBUKA KIDEDEA
Timu ya titanic leo imewanyuka home boys kwa jumla ya bao 3-1 katika mashindano yanayoendelea ya kombe la upendo katika mchezo uliofanyika uwanja wa tandika mabatini jijini Dar es salaam.

Taitanic ndio walikuwa wa kwanza kuzifumania nyavu za home boys katika dk 5 tu ya mchezo kupitia kwa Mrisho timam bao lililodumu hadi mapumziko.

kipindi cha pili kilianza kwa timu zote kuonyesha shauku ya kutaka kupata bao na katika 61 maulid kudra aliisawazishia bao timu yake ya home boys hali iliyowapelekea wapinzani wao kuongeza kasi ya mashambulizi kwa lengo la kupata ushindi katika mchezo huo.
Baada ya dk 6 mbele mrisho tamim tena aliipatia timu yake ya titanic bao la pili kabla ya Hebu Gamba kuongeza bao la 3 lililodumu hadi mwisho wa mchezo na kuwafanya home boys waondoke uwanjani kwa kichapo cha bao 3-1.

Kesho ligi hiyo itaendelea tena kwa kuzikutanisha timu ya temeke squad watakaotoana jasho na aman fc katika uwanja huo huo wa tandika mabatini.

Wakati huohuo timu ya sekondari ya magnus inatarajiwa kushuka dimbani kesho kumenyana na timu ya wakuzuka fc katika mchezo wa nusu fainali jez cup katika mchezo utakaofanyika katika uwanja wa majohe

Habari hii ni kwa mujibu wa mweka hazina msaidizi wa chama cha soka la vijana wilaya ya ilala IDYOSA

No comments:

Post a Comment