Saturday, August 8, 2009

YANGA KUUMANA NA MTIBWA SUKARI

Mabingwa wa soka nchini Dar yanga Afrikan wanatarajiwa kuchuana na mtimbwa sukari katika pambano la ngao ya hisani katka mchezo utakaofanyika jumapili wiki ijayo katika uwanja wa uhuru jijini Dar es salaam.

Katibu mkuu wa shirikisho la soka nchini tff Fredrick Lameck Mwakalebela amesema kuwa mchezo huo utakuwa ni sehemu ya maandalizi ya ligi kuu Tanzania bara inayotarajiwa kuanza kutimua vumbi august 23 mwaka huu.

Mwakalebela ameongeza kuwa mchezo wa ngao ya hisani utakuwa unafanyika kila mwaka ikiwa ni sehemu ya kuashiria kufungua kwa msimu wa ligi nchini


TIKETI KUWAONA SIMBA,VILA ZAUZWA
Tiketi kwa ajili ya pambano la simba na spot clab villa ya Uganda zimeanza kuuzwa leo katika vituo mbalimbali vilivyoteuliwa jijini Dar es salaam.

Kiingilio cha juu kabisa katika pambano hilo litakalofanyika kesho katika uwanja wa uhuru kitakuwa shillingi elfu 50 wakatik kile cha chini kitakuwa shilingi elfu 3.

Mwenyekiti wa kamati ya mashindano ya simba Hassan Hassano maarufu kama mpiganaji amevitaja vituo vya kuuzia tiketi kuwa ni katika vituo vya steers, hadees, big bon, millennium tower na maeneo mengine jijini DAR

Hassano ameongeza kuwa maandalizi katika tamasha hilo ambalo lina lengo la kuwatambulisha wachezaji wa simba ikiwa pamoja na kutambulisha jassey watakazotumia katika ligi kuu msimu ujao yamekamilika kwa asilimia kubwa.

Hasano amesema kuwa vifaa kwa ajili ya kupamba tamasha hilo vimewasili kutoka nchini afrika kusini hivyo amewataka mashabiki wa simba kujitokeza kwa wingi kesho uwanjani kushuhudia vitu vilivyoandaliwa na wekundu hao.

Sambamba na hilo clab hiiyo leo imetembelea katika hospitali ya taifa ya muhimbili kwa ajili ya kuwaona wagonjwa katika word ya watoto na wamefanikiwa kutoa zawadi mbalimbali kwa walengwa.


Katibu mkuu wa shirikisho la soka nchini tff Fredrick Mwakalebela amesema kuwa maandalizi kwa ajili ya michezo ya ufukweni inayofadhiliwa na shirikisho la soka ulimwenguni yaani fifa yanaendelea vizuri ikiwa pamoja na wadhamini mbalimbali kuanza kujitokeza

Mwakalebela amesema kuwa kwa sasa wanaandaa viwanja vitakavyotumika kaatika michezo hiyo.

UKATA WA YANGA HATIMAYE WAISHA
Baada ya kilabu ya yanga kuwa katika hali ngumu kiasi cha wapinzani wao kuanza kuwabeza kuwa wamefulia hatimae wachezaji wa wanajangwani hao wamelipwa malimbikizo ya mishahara yao ya miezi miwili.

Mmoja wa wachezaji hao ambae hakutaka jina lake litajwe redioni amesema kuwa kwa sasa karibu wachezaji wote wana ari ya kufanya mazoezi baada ya adui njaa kuanza kuwakimbia.

Ameongeza kuwa amekuwa katika wakati mgumu sana kiuchumi kiasi ambacho hawezi kukielezea na kuongeza kuwa anaushukuru uongozi wao kwa kuweza kulifanyia kazi suaala hilo mapema iwezekanavyo.

Ameongeza kuwa kwa sasa anaamini mazoezi ya wanajangwani hao yataendelea vizuri japo wachezaji sita wa timu hiyo wapo katika kikosi cha taifa stars kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa kirafiki dhidi ya amavubi ya Rwanda utakaofanyika wiki ijayo nchini Rwanda.

Wachezaji hao walikuwa wakidai mishahara yao ya miezi miwili juni na julai hali iliyopelekea kudorola kwa mazoezi hayo na kumfanya kocha mkuu wa timu hiyo Dusan Condic kuwa katika wakati mgumu wa kuendelea na programu yake ya maandalizi ya ligi kuu.

KIFA KUWAPATA KINONDOKE KESHO
Uchaguzi wa chama cha makocha mkoa wa kinondoni kisoka unatarajiwa kufanyika jumapili wiki hii katia ukumbi wa manspaa ya kinondoni huku nafasi ya mweka hazina msaidizi ikiwa wazi kwa kukosa mgombea.

Katibu mkuu wa chama cha soka kinondoni KIFA Frank Mchaki amesema kuwa usaili kwa ajili ya uchaguzi huo umeshafanyika na kupitisha wagombea waliokizi vigezo.

Mchaki amewataja wagombea watakashiriki katika uchaguzi kuwa ni Eliutel Mholela katika nafasi ya mwenyekiti, wakati makamu mwenyekiti ni Cansius Masombora.

Nafasi ya katibu mkuu itagombewa na Mbwana Makata wakati nafasi ya katibu msaidizi yupo Daniel Mashote

Mweka hazina itagombewa na Evarist Katomondo huku nafasi ya mweka hazina msaidizi ikiwa haina mgombea.

Boniface Wambura atagombea nafasi ya mjumbe taifa wakati Hamis Pondamali na Samson Hika wao watagombea nafasi ya mjumbe kamati ya utendaji.

No comments:

Post a Comment