Friday, February 6, 2009

Kuishi kwingi kuona mengi,mgaa na upwa hali wali mkavu,na kuti la mazoea humwangusha mgema.sikusudi langu kufundishana methali au kuandkika methali hizi katika hii makala bali ni kutaka kutumia kama sehemu ya semi zitakazokamilisha kile nilichokipata hapa kwa muda wa siku tano kuanzi jumatatu hadi leo ijumaa.

Ilikua kama mzuka nilipopata mwaliko wa kuhudhulia wordshop hii kupitia MISA Tanzania.hakika nilijua kwa namna moja a u nyingine mimi najua kutokana na elimu niliyonayo kuhusinana na mambo ya internet nikadhani nafahamu karibu kila kitu kumbe nilikua najidanganya katika mambo ya internet kama ni bahari basi nafahmu ujazo wa lita elfu kumi tu.

Workshop hii imebadili sana mwelekeo wa kuweza kupata taarifa zangu,tangu jumatatu nilipofika hapa na kuanza kujifunza mambo ya internet nilianza kufamu mambo mengi zaidi.moja wapo ya mambo niliyojifunza ni pamoja na namna ya kuweza kutafuta habari kutoka vyanzo mbalimbali vya habari.kupitia mtandao unaweza kupata makitaba mbalimbali ulimwenguni,namba za simu za wwatu na mashirika mbalimbali,musiki na wasanii pamoja na historia zao.na burudani mbalimbali.

Mbali na habari unaweza,unaweza kuweka oda mbalimbali ikiwa pamoja na kununua kuuza vitu kupitia mtandao.baadhi ya mitandao ambayo nilikuwa ssiijui na ni vyanzo vya habari ni kama vile slash,salon,internet usage,alexa, youtube na amazon.

Mbali na hayo nimeweza kujua pia namna ya kuweza kufungua tovuti yangu mwenyewe kitu ambacho nilidhani ni kazi kubwa sana ambayo ilihitaji watu maalumu tu




au au makampuni tu.lakini leo hii unaweza kupata habari yangu kupitia mtandao wangu mwenyewe ujulikanao kama bugobora na kuweza kupata habari mbalimbali ambazo mimi mwenyewa nimeziandaa.

Napenda nitoe shukurani zangu za zati kwa MISA- Tanzania ambao nia waandaaji wa workshop hii pamoja na mkufunzi wetu ndugu PEIK JOHANSSON Kutoka Finland kwa jinsi ambavyo ameweza kutufungua na kutuwezesha kutambua vitu mbalimbali kutitia mtandao.kupitia sisi hakika kampuni zetu tunazoziwakilisha zimenufaika vya kutosha,na kile tulichokipata kitakua chachu pia kwa wenzetu ambao tunafnya naokazi.

Mapendekezo yangu semina hii ingeendelea kutolea japo kwa muda wa mwezi mmoja

No comments:

Post a Comment